Siku zote majibu ya maswali mengi yanapatikana tukiwa tukijiuliza, je hivi ni kwanini inakuwa hivi? au je kwanini isiwe hivi? Basi pale utakapo anza kujiuliza haya maswali mara nyingi utapata majibu!
Jinsi nilivyo anza na hayo maneno hapo juu ni kwamba nataka kuzungumzia kuhusu swala ambalo nataka tuweze kunufaika sote wana-blog ambapo Mara nyingi ukiangalia blog zetu utakuta kuna msululu wa archives, msululu wa previous posts (Last posts) basi inaleta karaha kubwa (Picha Mbaya) kutokana na hiyo misululu na hii inaendana na kama mtu ukiwa una posts nyingi za zamani!
Pia tukiangalia blog zetu ktk Archives siku zote posts zile mpya zinakuwa chini na za zamani zinakuwa juu sasa baada ya kuweka code mpya za leo zitakufanya blog yako iwe na uwezo wa kuonesha ktk Archives Post mpya kwanza na kufuatia na post za zamani!!
Sasa jawabu la hilo swali au tatizo mwisho wake ni leo 25th April 2006 11:19:30am GMT+1 ambapo nakuja na code ambazo zitaondoa kabisa hiyo misululu isiyo kuwa na mwisho!
Yafuatayo ni maelekezo ya kufanya:
1: Sign In ktk Blog yako.
2: Ukifika ktk Dashboard, Click Change Settings alafu tena click Template.
3: Ukiwa ndani ya Template tafuta wapi yalipo haya maandishi,haya ni maandishi yaliyopo ktk template yangu sasa nina uhakika asilimia 99.99 ya kwamba ktk blog zenu kutakuwa na kitu kama hiko hiko. kwa kifupi, haya maandishi yapo mwisho mwisho wa code za blog zenu sasa mkifika ktk template nenda chini (mwisho wa code) na uanze kuangalia wapi hayo maandishi yalipo.
4: Baada ya kuyapata, Badilisha (Futa) maandishi yoyote yanayo endana na Archives au Previous Post (Last Posts) na nawaomba muweke hizi code.
Hizi code ni za Archives pamoja na Previous Posts (Last Posts) sasa ukiwa unafuta code kumbuka kuweka code zitakazo kwenda kuziba pengo lililowachwa wazi pia kuwa muangalifu usije kufuta code zisizo endana na Archives au Previous Post (Last Posts).
Kama kukiwa na tatizo au maswali yoyote nitafurahi kuweza kuyajibu au kutoa ushauri wowote, cha kufanya ni kuniandika hapa ktk hii blog au nitumie e-mail na nitakujibu asap.
Nashukuru.
2 comments:
E bwana hii page ulioisema ina hizi codes haipatikani sijui tatizo nini kwa hiyo tusaidie kwa hilo.
Aha Samahani nilikuwa bado sija-upload sasa hivi hipo tayali unaweza kuangalia. Nakutakia kazi njema.
Nashukuru kuweza kutembelea hii blog.
©2006 MK
Post a Comment