Sunday, May 07, 2006

JE UNAMJUA GARY MCKINNON?
Gary Mckinnon kwa jina lingine anajulikana kama Solo (Miaka 39) ni hacker raia wa Uingereza ambaye ktk historia za ma-hacker anajulikana kama ni mtu pekee aliyeweza ku- hack computer 97 muhimu sana za jeshi la Marekani na computer za NASA kati ya mwaka 2001 - 2002, Nikizungumza Jeshi la Marekani nina maanisha majeshi yote ya Marekani.

Gary Mckinnon aliweza kukamatwa mwaka 2002 baada ya kugunduliwa na kikosi cha uingereza kijulikanacho kama National Hi-Tech Crime Unit (NHTCU) na alikamatwa kutokana na sheria ijulikanayo kama Computer Misuse Act.

Hivi sasa bwana Gary Mckinnon yupo nje kwa masharti ya kwamba kila siku jioni ni lazima aweze ku-report ktk kituo cha polisi, Haruhusiwi kutumia Computer yoyote ile yenye huduma ya Internet, na ni lazima kila siku alale nyumbani kwao.

Mpaka sasa kesi inaendelea nchini Uingereza na Serikali ya Marekani imeiomba Serikali ya Uingereza impeleke bwana Gary Mckinnon nchini Marekani waweze kumshitakia ndani ya Marekani, Kama akipelekwa Marekani na kupatikana na hatia anakabiliwa kufungwa si chini ya miaka 70 ndani ya jela.

Kama unataka kuangalia video yake ikimuonesha akielezea jinsi alivyo fanya hayo mambo naomba bonyeza hapa.

Mwisho, Ndugu wasomaji nawaomba muwe makini na watu kama hawa na siku zote akikisha computer zenu zina ulinzi wa kutosha sababu kama mtu huyu ana uwezo wa ku-hack computer za Serikali ya Marekani basi watu kama hawa wana uwezo wa ku-hack computer zetu, za Serikali yetu na mashirika yote ndani ya Tanzania.

Kwa habari zaidi endelea kutembelea Vijimamboz

2 comments:

Jeff Msangi said...

MK,
Hili nilikuwa silijui kwa hiyo ahsante kwa kunifumbua.Lakini suala la matumizi ya kompyuta yenye internet sio suala la haki za binadamu hili kweli?Nitajaribu kuifuatilia zaidi hii kesi.

Reggy's said...

MK habari za leo. Nimepata challenge kuhusu KIJIWE CHA GHAHAWA. Wanaotembelea kijiwe changu wanabanwa mbavu. naomba unisaidie kukipanua, ili kila anayeingia aweze kutoa maoni hadi yaishe badala ya kuandika na kubanwa na character 200 tu.
Nawasilisha!