Wednesday, April 05, 2006

JAWABU LIMEPATIKANA:

Baada ya kukaa chini muda mrefu na kuweza kugundua code zinazo ondoa Blogger NavBar (Ile Search Box iliyopo juu ya blog yako) hii ni kutokana watu wengi hawaipendi Blogger NavBar. lakini kutokana ya kwamba hakuna njia nyingine ya mtu ku-search kwa urahisi nakala ulizo andika nyuma (zilizopita) ilibidi watu wengi waache Blogger NavBar kama ilivyo!!

Sasa nimerudi tena na kuweza kugundua code mpya zitakazo wezesha mimi na wewe kuondoa Blogger NavBar na vile vile kuendelea kuwa na uwezo wa ku-search nakala zako zilizo pita.

Yafuatayo ni maelekezo ya kufanya hivyo:

A: Fanya yale maelekezo niliyo andika mwanzo ili uweze kuondoa Blogger NavBar naomba usome kupitia hapa. , Baada ya kuweza kuondoa Blogger NavBar fuata haya maelekezo:

B: Copy code zifuatazo (Chagua moja wapo la kundi yafuatayo hapa chini kutokana na mapendekezo yako) na nenda ktk Sign in ktk Blog yako-->Dashboard-->Change Settings-->template na uweze kuchagua ni mahali gani unataka hii Search Box yako iweze kutokea. Baada ya kuchagua na kupata sehemu ya kuweka code zako (sehemu ya kutokea search box yako) Paste code ulizo zi-copy. Kama unataka kuona search box yako imekaa sehemu unayo itaka (unayo ipenda) click Preview kabla ya ku-click Save Template Changes au ku-Click Republish your Blog. Endelea kufanya hivyo mpaka utakapo pata sehemu unayo ipenda.

C: Katika hizi code utakuta neno YOUR DOMAIN NAME futa hayo maandishi na weka anuani ya website yako yaani mfano: value="YOUR DOMAIN NAME" name.. na iwe hivi: value="http://vijimamboz.blogspot.com" name hivyo ndio mfano kama ingekuwa ni mimi naweka hizo code sasa badilisha kutokana na anuani yako ya blog. Fanya hivyo popote pale utakapo ona hilo neno ktk code zifuatazo hapa chini.

D: Click Save Template Changes alafu Click Republish your Blog.

Kutokana ni vigumu kuweza kuweka hizo code hapa maana zinakataa kuji-publish na kutokea kama page, nawaomba msome kupitia hapa. (Right click na chagua open in new window) ili ifunguke ktk page nyingine.

utaitaji ms-word kufungua hili file.

Kumbuka watu wengi hawaipedi Navbar kutokana inazuia kuweza kuweka vitu vingi ktk site yako mfano: calendar, saa na vitu vingi ambavyo vinaitaji viwepo juu ya site yako, Vile vile inaleta picha mbaya.

Kama una maswali au Tatizo zaidi kuhusu hili swala naomba niandikie na nitakujibu asap.

Nashukuru.

4 comments:

Anonymous said...

Nashukuru kwa dawa, mimi nimeitumia na imenitibu. Nitaendelea kukosoma MK

Anonymous said...

safi sana kaka.paul

Anonymous said...

MK kazi ya kuja na utaalamu wa teknolojia ya kompyuta kila kukicha naifurahia sana. Hongera sana. Hivi hii ya kuweka viunganishi kwenye comment unapatikana vipi kwenye blogspot.com?

Anonymous said...

Samahani kwa kutokujibu swali lako mapema sababu ndio leo naliona. Lakini ndugu Mwaipopo sijakupata vizuri ktk swali lako hivyo basi ninakuomba uweze ukarudia tena kuniuliza kwa undani zaidi ili nielewe au niandikia kwa undani ktk e-mail na nitakujibu asap.

Samahani kwa usumbufu uliojitokeza.

Nashukuru kwa kutembelea Vijamamboz. Karibu tena.

©2006 MK