Monday, April 03, 2006

Baada ya uchunguzi wa siku nyingi na wa hali ya juu nimegundua jawabu la kuondoa Blogger NavBar (Sehemu ya juu kabisa ya Blog yako inayo onesha search this blog). Hii kutokana na ya kwamba watu wengi uwa wanachukizwa na jinsi hiyo NavBar ilipo.

Jawabu la hili swali ni:

1: Sign in ktk Blog yako.

2: Ukifika ktk Dashboard, Click "Change Settings" alafu Click sehemu ya "Template".

3: Ukishafika kwenye Template tafuta wapi yalipo haya maandishi:
link rel="stylesheet" type="text/css" href="style.css"/>
/*

au blog zingine kuna maandishi haya:
style type="text/css"
/*

Hapa kwenye template ni sehemu inayo ifadhi code ambazo zinazotengeneza blog yako. Sasa basi mara nyingi hayo maandishi yapo mwanzo mwanzo wa code zinapoanzwa kuandikwa. Sasa usiangaike kwenda chini zaidi au katikati, Wewe Unapofika kwenye template tu angalia mwanzoni na utaona hayo maandishi.

4: Baada ya kupata hayo maandishi naomba chini yake weka haya maneno: #b-navbar{ margin-top: -500px;}

Kumbuka haya maneno ndio dawa ya kuondoa NavBar. Narudia tena dawa ni #b-navbar{ margin-top: -500px;}

Baada ya kumaliza ni lazima maandishi yaonekane kama hivi:
link rel="stylesheet" type="text/css" href="style.css"/>
#b-navbar{ margin-top: -500px;}
/*

Wenye blog zingine zionekane kama hivi:
style type="text/css"
#b-navbar{ margin-top: -500px;}
/*

5: Mwisho: Click Save Template Changes alafu Click Republish your Blog.

Kama una maswali au Tatizo zaidi niandikie.

Nashukuru.

14 comments:

Martha Mtangoo said...

Haki ya nani hilo somo mbona linaonekana gumu? unajua nimejaribu nimeshindwa sijui nifanyaje sasa, jaribu kurudia kuelekeza mimi nimeshindwa.

MK said...

Samahani Dada yangu Martha Beatrice Mtangoo kwa jinsi blog yako ilivyo tengenezwa, Basi nenda kwenye hii sehemu:

style type="text/css"

Baada ya kuyapata hayo maneno, Alafu kwa chini yake ndio weka hiyo dawa niliyo sema.

Kwa wengine wote wenye maswali naomba mniulize maana blog zenu zinautofauti yaani kila blog zimetengenezwa tofauti.

MK said...

1: Sign in ktk Blog yako.

2: Ukifika ktk Dashboard ( Dashboard Inaonekana kama hivi), Click "Change Settings" alafu Click sehemu ya "Template".

3: Ukishafika kwenye Template tafuta wapi yalipo haya maandishi:
style type="text/css"

Baada ya kupata hayo maandishi naomba chini yake weka haya maneno: #b-navbar{ margin-top: -500px;} kama yalivyo.

Kumbuka haya maneno ndio dawa ya kuondoa NavBar. Narudia tena dawa ni #b-navbar{ margin-top: -500px;}

Mwisho: Click Save Template Changes alafu Click Republish your Blog.

Kama una maswali au Tatizo zaidi niandikie.

Naomba nijibu kama umefanikiwa.

Nashukuru.
©2006 MK

Imetengenezwa na kuletwa kwenu na ©2006 MK

boniphace said...

safi sana kazi nzuri hii haya Magazeti Tando yetu yanataka kuwa na vivutio hivi ili kuyafanya yasomeke zaidi. Kazi safi sana MK nitapita nikipata muda kuchukua ujuzi

John Mwaipopo said...

Nashukuru MK kwa ufundi na taarifa yako. Nimekuwa na shauku ya kujua vitu fulanifulani. Sasa nitakua nikikuuliza. Asante sana.

Jeff Msangi said...

Ahsante kwa hili..nimejaribu na kufanikiwa mara moja kuondoa kile kiwingu pale juu...asante na kazi njema.

Anonymous said...

MK,
Asante kwa kutoa ushauri kwa wanablogu. Nimemaliza kuandika pale kwenye blogu ya Jeff kuhusu huu ufito wa juu wa Blogger. Nimemwambia kuwa moja ya faida za ufito ule, hasa kwangu (sijui kama wasomaji wengine wanautumia) ni kusaka habari za nyuma (pale panaposema "search this blog"). Hii imekuwa ikinipunguzia muda na ugumu wa kupata habari kwa kuweza kusaka habari zilizoko ndani ya blogu na sio kusaka habari zilizoko kwenye Intaneti nzima. Nikamwambia Jeff, ambaye ameondoa ule ufito, kuwa itabidi kama watu hawautaki ule ufito, basi tujaribu kuwa na ufito au sanduku la kuwezesha wasomaji, hata mwenye blogu mwenyewe, kusaka habari zilizoko ndani ya blogu kama ilivyo hao kwenye ufito wa juu.

Hata jana nimetumia ufito huu kwenye blogu ya Michuzi kutafuta habari zote ambazo amewahi kumtaja Jeff. Na nikazipata kwa sekunda chache kutokana na ufito ule.

Umenipata?

Anonymous said...
This comment has been removed by a blog administrator.
Anonymous said...

Nashukuru Muheshimiwa Ndesanjo kwa maoni yako lakini watu wengi walikuwa wakiniuliza kuhusu hiyo search box maana mtu unashindwa kuweka baadhi ya vitu fulani juu ya page yako.Alafu watu wengi ina wakera sana!

Kuhusu kutafuta habari mbona kuna section ya Archives ambayo inaonesha nakara zote zilizopita.Sasa kama mtu unataka nakara zilizo pita click hapo na utaziona.

Nimeamua kugundua hizo code kwa kuwapa watu uhuru wa kuweka vitu kama tarehe, saa na n.k kama unavyo ona page yangu ilivyo.

Nashukuru Muheshimiwa kwa Maoni yako.
©2006 MK

Anonymous said...

MK,
Tatizo la Archive ni moja. Ngoja nikupe mfano. Majuzi nilikuwa natafuta picha na habari aliyotupa Mwandani iliyosema: Tanzania Business Community. Sasa ukiwa hukumbuki tarehe na mwezi ambao aliandika habari hiyo ukienda kwenye "archive" hutatumia muda mrefu sana kuipata. Ukitazama "archive" ya blogu ya Jeff utaona ina tarehe, miezi, na mwaka. Je habari aliyoandika ambayo hukumbuki mwezi na mwaka utaipata vipi? Utakuwa kama mtu anatembea kizani.
Jaribu kwenda kwa mwandani: http://mwandani.blogspot.com
kisha nenda pale kwenye ufito wa juu. Andika maneno haya: tanzania business community kisha bonyeza kwenye "search this blog" utaona unaipata habari hiyo mara. Lakini kwa kupitia kwenye "archive" ni vipi utaipata habari hiyo kwa muda mfupi hivyo?

Nadhani kama mtu anataka kuweka vitu pale juu au hapendi ufito ule anaweza kubadili. Ila nilitaka tu kusema kuwa ufito ule unatusaidia wasomaji kwa kiasi fulani.

Halafu kuna kile kibendera pale kwenye ufito ambacho kazi yake ni kutoa taarifa kwa blogu ambazo zinatumiwa labda kinyume cha sheria au maadili. Kinaweza kuwa hakina kazi kubwa kwenye blogu zetu kwa sasa, ila kimesaidia kwenye matukio fulani fulani. Ila hili sio kubwa kwangu kama uwezo wa kupata mambo yaliyoandikwa huko nyuma kwa urahisi bila kuanza kubuni mwezi na tarehe ambayo habari hiyo iliandikwa.

Anonymous said...

Ni maoni mazuri ndugu yangu ndesanjo ambayo kutumia mawazo mazuri kama haya ndio yanayo fanya tuendelee zaidi.

Hivyo basi kutokana na maombi yako nimeweza kutengeneza code ambazo zinalingana na maombi yako ambayo utayaona mwanzo wa site hii.

Nashukuru sana muheshimiwa ndesanjo na tuzidi kupeana ushauri zaidi ili kudumisha hizi blog zetu.

Kingine naomba niulize huko ulipo hivi mnaiona vijimamboz player hapo juu kwa uzuri? Maana nataka kufahamu kuhusu hili.

Nashukuru,
©2006 MK

Anonymous said...

Ndio MK,
Unajua maoni yako yenye ushauri juu ya kuondoa ule ufito yalichukuliwa na blogu yangu kama ni "spam." Nimeshairuhusu itokee na kuwa sio "spam." Nikitumia firefox mozilla lazima nishushe "plugin" ndio nitaweza kuona. Kwenye internet explorer ambayo siitaki kabisa player haina matatizo.

Anonymous said...

Safi sana

MK utundu na ugunduzi wako umetusaidia sana mimi niliposoma tu maelezo yako nikayafuatilia kwa kina na nikauondoa ufito, sasa itabidi tusaidie njia mbadala labda kwa mfano ile search ikae kwa chini siyo juu.

Otherwise itakuta nikikutembelea katika hili kasri lako kuomba msaada wa kina maana mambo yanaonekana kwako kuwa supa zaidi kadri tunavyosonga mbele.

Anonymous said...

Nashukuru ndugu yangu, nimesikia maoni yako na nashukuru kuona mnatembea hii blog.

Ukiwa na shida au swali ktk swala lolote naomba niandikie ktk e-mail au niachie ujimbe hapa na nitakujibu asap.

Nashukuru sana,
©2006 MK