Thursday, June 15, 2006

UPUNGUFU WA MAJI ULIMWENGUNI NI CHANZO CHA VITA YA BAADAE.
Uhalibifu wa mazingira na vyanzo vya maji pamoja na harakati za kibinadamu ktk kujitafutia maendeleo kutokana na majaribia mbali mbali yanayo haribu mazingira ni vyanzo vikuu vikubwa vinavyo sababisha upungufu wa maji ulimwenguni.

Kama ilivyo kwa thamani ya bidhaa za madini mbali mbali, Petrol, Diesel pamoja mafuta ya taa ambayo inayo fanya au kuleta vita hapa duniani ndivyo itakavyo kuwa ktk hii bidhaa muhimu (maji) ktk maisha ya binadamu ambayo ina muwezesha kuweza kuishi na hapo ndipo binadamu tutaweza kupigana vita kwa sababu ya upungufu wa maji.


Kama binadamu wa sasa hawezi kutunza mazingira yake pamoja na vyanzo vya maji basi matatizo makubwa yanaweza kutukumba, Baadhi ya hayo matatizo tunayaona sasa ambapo kila kona ya ulimwengu kuna upungufu wa maji. i.e Kama tunavyo fahamu uchumi wa nchi nyingi ulimwenguni unategemea kilimo ambapo hiko kilimo kinategemea maji sasa kama hakuna maji basi uchumi wa mataifa mengi utakuwa mbaya ambapo utazoretesha uduma mbali mbali za kijamii, n.k

Nawaomba muangalie hii habari kuhusu matatizo ambayo tunayo na yatakayo tukumba.

Mwisho, tuweze kutunza mazingira yetu na kuweza kuelimisha jamii nzima kuhusu mazingira na tuweze kutumia maji tuliyo nayo kwa uangalifu.

Thursday, May 18, 2006


HISTORIA YA AIRBUS A380 NDANI YA UK
Ndege ya abiria aina ya Airbus A380 yenye viti vya abiria 555 ambayo ni kubwa kuliko zote ulimwenguni imeweza kuingia ktk historia ya kuwa ni ndege ya kwanza ya aina hiyo kutua ktk ardhi ya Uingereza ktk uwanja wa ndege wa Heathrow hii leo 18/05/2006 saa 13:20 mida ya Uingereza ikitokea Berlin, Germany.

Maandalizi ya kuwezesha ndege hiyo kutua ktk uwanja wa Heathrow imewagarimu waingereza ( British Airports Authority) jumla ya 450 Million pounds na pia imetua ktk sehemu impya ( Inayo julikana kama pier 6 ktkTerminal 3) iliyo jengwa na kugarimu jumla ya 105 Million pounds.

Airbus A380 itakuwa ni mshindani mkubwa wa ndege za Boeing, na kuonesha Boeing wapo ktk ushindani nao wametengeneza ndege aina ya 787 Dreamliner kuweza kushindana ambayo inategemewa kuingia ktk soko ifikapo mwaka 2008 na kuweza kubeba abiria kati ya 200 mpaka 350.

Jumla ya gharama zilizo wezesha kutengeneza ndege ya Airbus A380 ni 6 Billion pounds ambapo mpaka sasa kampuni ya Airbus S.A.S imepokea order karibia 159 kutoka kwa mashirika 16 ya ndege zinazotaka kununua aina hii ya ndege.

Bonyeza hapa kusoma orodha ya makampuni na idadi ya ndege walizo order.

Bonyeza hapa kuona video mbali mbali za Airbus A380 pia kama ukitaka kuangalia video nyinginezo zinapatikana kwa kubonyeza hapa.

Mwisho, ingawa hii ni kama historia lakini imeleta mitazamo tofauti ambapo kuna makundi mawili, yanayo kubaliana na technology hii na wanao ipinga kutokana na sababu za mazingira.

Tuesday, May 16, 2006

Kama ukitaka blog yako ipendeze zaidi, basi unaweza kuweka hizi code ili kuweza kufanya scrollbar yako kubadilika rangi au iwe na rangi tofauti tofauti. Unaweza kuangalia scrollbar ktk blog yangu na kuona ninacho sema.

Unaweza kubadili rangi tofauti tofauti kutokana na mapendekezo yako, na utaweza kufanya hivyo ktk sehemu zenye maandishi kama #FFFFFF; #6DA4FF; #ACA899; black; #FFFFFF; na kufuta #FFFFFF, #6DA4FF, #ACA899, black au #FFFFFF na kuandika rangi unayotaka eidha kwa kutumia code kama nilivyo andika mwanzo au kwa maandishi mfano pink, green, red, n.k.

Kumbuka ukiandika kwa code au kwa maandishi andika kwa usahii na kwa kiingereza tu na msifute alama hii ; yaani ukiandika red iwe red; au #ff0000; hivyo ndivyo ingekuwa kwa kutumia code nikiwa nina maanisha rangi nyekundu.

Yafuatayo ndio maelekezo ya kufanya:

1: Sign In ktk Blog yako

2: Ukifika ktk Dashboard,Click->Change Settings->Template

3: Ukifika ktk template, tafuta wapi yalipo haya maandishi head yakianza na tag < na kuishia na tag > na baada ya kuyapata hayo maandishi chini yake weka code zifuatazo.

4: Mwisho, click save template changes alafu click republish your blog.

Na hapo utakuwa umemamaliza kila kitu.

Tuesday, May 09, 2006

NA NYINGINE HIYO!!
Leo nawaletea code nyingine kwa wale wenye blog ndefu au blog za picha ambazo ni ndefu.

Code hizi ni kuwawezesha wasomaji wenu kuweza kupelekwa juu (Mwanzo) pale wafikapo mwisho bila ya kuangaika kwenda juu. Mfano wake upo ukiangalia chini ya hii blog (Vijimamboz) utaona kuna kijisehemu kina kwambia rudi juu na uki-click hapo unakwenda juu.

Maelekezo ni kama kawaida, Ambayo ni:
1(a): Sign In ktk Blog yako

1(b): Ktk Dashboard,Click->Change Settings->Template

1(c): Ukifika ktk template, Chagua ni wapi unataka hiyo button iweze kukaa (Ni vizuri ukiweka chini kabisa maana wasomaji wenu wakishafika mwisho wa blog tu waweze kukibonyeza na kupelekwa juu) na alafu muweke hizi code.

1 (d): Mwisho, click save template changes alafu click republish your blog.

Na hapo utakuwa umemamaliza kila kitu.

Sunday, May 07, 2006

JE UNAMJUA GARY MCKINNON?
Gary Mckinnon kwa jina lingine anajulikana kama Solo (Miaka 39) ni hacker raia wa Uingereza ambaye ktk historia za ma-hacker anajulikana kama ni mtu pekee aliyeweza ku- hack computer 97 muhimu sana za jeshi la Marekani na computer za NASA kati ya mwaka 2001 - 2002, Nikizungumza Jeshi la Marekani nina maanisha majeshi yote ya Marekani.

Gary Mckinnon aliweza kukamatwa mwaka 2002 baada ya kugunduliwa na kikosi cha uingereza kijulikanacho kama National Hi-Tech Crime Unit (NHTCU) na alikamatwa kutokana na sheria ijulikanayo kama Computer Misuse Act.

Hivi sasa bwana Gary Mckinnon yupo nje kwa masharti ya kwamba kila siku jioni ni lazima aweze ku-report ktk kituo cha polisi, Haruhusiwi kutumia Computer yoyote ile yenye huduma ya Internet, na ni lazima kila siku alale nyumbani kwao.

Mpaka sasa kesi inaendelea nchini Uingereza na Serikali ya Marekani imeiomba Serikali ya Uingereza impeleke bwana Gary Mckinnon nchini Marekani waweze kumshitakia ndani ya Marekani, Kama akipelekwa Marekani na kupatikana na hatia anakabiliwa kufungwa si chini ya miaka 70 ndani ya jela.

Kama unataka kuangalia video yake ikimuonesha akielezea jinsi alivyo fanya hayo mambo naomba bonyeza hapa.

Mwisho, Ndugu wasomaji nawaomba muwe makini na watu kama hawa na siku zote akikisha computer zenu zina ulinzi wa kutosha sababu kama mtu huyu ana uwezo wa ku-hack computer za Serikali ya Marekani basi watu kama hawa wana uwezo wa ku-hack computer zetu, za Serikali yetu na mashirika yote ndani ya Tanzania.

Kwa habari zaidi endelea kutembelea Vijimamboz

Saturday, May 06, 2006


NI NANI WA KUOKOA DARFUR NA AFRIKA?

Hapa uliwenguni ni mahali pazuri na pabaya kuishi, Ni pazuri kama tukiwa na Amani na Upendo na Vile vile kunakuwa ni pa chungu kama Amani na Upendo ukitoweka.

Dhumuni la nakala hii ni kuonesha au kuuliza ni nani atakae okoa Wananchi Darfur na Afrika kwa ujumla hasa hasa watoto na akina Mama? Kwa Mfano hapo Darfur ni tatizo la siku nyingi likiwa linaendelea kila siku na Viongozi wetu wa hii dunia wakibaki kuliangalia tu kama vile hawalioni!! Wanabaki wakiliangalia na kuacha ma-million ya wananchi wakiteseka na kufa kwa njaa au kuuana wenyewe kwa wenyewe.

Vile vile hata Serikali yenyewe ya Sudan inabaki midomo imefunga na kuliangalia hilo swala ata pia wakiweza kudhamini ata wale magaidi (The Janjaweed) wanao ua kila siku watoto, wanawake, na wanaume!!

Nchi nyingi za Afrika wanajifanya kama hawalioni hili swala na kuna wakati walijifanya wanaona na kupeleka majeshi ya AU (Askari 7,000 tu) lakini cha kushangaza hayo majeshi hayafanyi chochote kuzuia Vifo vya watoto, wanawake, na wanaume.

Dunia inajifanya inaona na kutaka kusaidia lakini inapofika kusema kuiwekea Serikali ya Sudan Vikwazo na kupeleka majeshi ya UNO kulinda Amani, Utaona baadhi ya nchi zinazopata maslahi toka Sudan zikizua hilo pendekezo hii ikijumuisha nchi ya China ambayo imewekeza zaidi ya 3 Billion US Dollars ktk Mafuta ya Sudan na hizo hizo pesa ndizo zinazo dhamini Silaha zinazo leta hivi Vifo.

China imekuwa nchi ambayo haifuati haki za binadamu na Sheria ambapo kutokana siku hizi imekuwa Super Power ktk hii dunia basi matumizi yake pia yanakua ambayo yanafanya kutafuta soko la mahitaji yake bila hata ya kufuata sheria (Kufumba Macho mabaya yafanywayo na Serikali zinazo mpatia hayo mahitaji) hii ikijumuisha Kenya- Haikemei Rushwa inayo endelea, n.k, Zimbabwe- Haikemei uvunjwaji wa haki za binadamu, n.k, Sudan- Haikemei Uvunjwaji wa haki za binadamu, na pia ndio inazuia muswada usipitishwe ktk Umoja wa mataifa kwakuwa ina kura ya Veto, Chad- Haikemei uvunjwaji wa haki za binadamu na watu wanakufa na njaa huku kiongozi wa nchi hii akiishi maisha ya kifalme na kununua magari ya kifahari!! Hii mifano sio kwa nchi za Afrika tu bali ktk nchi nyingi hapa duniani, Yaani nina mifano mingi tu hii ikijumuisha mataifa mengi hacha China tu.

Mpaka nina andika hii nakala baadhi ya vikundi ndani ya Sudan havikuweza kuweka sahii ktk makubaliano ya Amani!!

Kwa Ufupi tu hapa nina uliza ni nani atakae kuja kutukomboa ktk haya matatizo tuliyo nayo Afrika?

Ni nani atakae kuja kuokoa watoto, Wakina Mama, Wakina Baba wa Darfur?

Kwanini wanaendelea kuuza Silaha kwa nchi za Afrika zenye machafuko zinazo fanya kuuana wenyewe kwa wenyewe?

Wako wapi Viongozi wa Afrika na hii dunia?

Mungu Ibariki Tanzania, Mungu Ibarika Afrika.

Nashukuru.

Wednesday, May 03, 2006

MAMBO MAPYA
Je ulishawahi kuwa na website au Blog na baadae ukaamua kutengeneza website au blog nyingine kutokana na sababu mbali mbali?

Kama jibu ni ndio ni wazi kwamba baadae uliweza kuwataharifu ndugu, jamaa na marafiki kama umebadilisha anuani ya website au blog ile ya zamani na kuamua kuwapa anuani mpya ili waweze kukutembelea ktk makazi mapya.

Sasa leo hii nakuja na code zitakazo kukuondolea tatizo la kuambia watu wote kwamba anuani yako ya website imebadilika, cha kufanya hapa ni kufuata malelekezo yafuatayo:
1(a): Sign In ktk Blog ile ya zamani

1(b): Ukifika ktk Dashboard, Click -->Change Settings-->Template

1(c): Ukifika ktk Template tafuta wapi yalipo haya maandishi head yakianza na tags < na kuishia na tag > na baada ya kuyapata hayo maandishi chini yake weka code zifuatazo, bonyeza hapa kuzipata.

2 (a) Utafanya hivyo hivyo ata ktk website yako ambayo ni tofauti na blog, Chakufanya nenda ktk sehemu zilipo code zinazo tengeneza website yako na tafuta maandishi head yakianza na tag < na kuishia na tag > ambayo yapo mwanzo mwanzo mwa code zilipo anzwa kuandikwa na uweke hizi code.

Kuna code za aina mbili ambazo kazi zake zote ni za aina moja sasa mtachagua ni code zipi mtazitumia ktk ya hizo mbili (Yaani chagua moja tu).
Ukikuta sehemu nimeandika "weka anuani mpya hapa" unabidi muweke anuani zenu za website au blog mpya mfano http://vijimamboz.blogspot.com hii ni kama ingekuwa mimi.

3: Mwisho, click save template changes alafu click republish your blog au wenye website tofauti na blog click Save changes.

Basi baada ya kumaliza hapo tu watu wakiwa wanaenda ktk ile website au blog ya zamani watapelekwa moja kwa moja katika makazi mapya ( Yaani ktk website au blog yako mpya).

Ukiwa na maswali zaidi kuhusu hii nakala naomba niandikie na nitakujibu asap.

Nashukuru.

Tuesday, April 25, 2006

SAA YA KUONDOA MSULULU NDANI YA BLOG NI SASA.

Siku zote majibu ya maswali mengi yanapatikana tukiwa tukijiuliza, je hivi ni kwanini inakuwa hivi? au je kwanini isiwe hivi? Basi pale utakapo anza kujiuliza haya maswali mara nyingi utapata majibu!

Jinsi nilivyo anza na hayo maneno hapo juu ni kwamba nataka kuzungumzia kuhusu swala ambalo nataka tuweze kunufaika sote wana-blog ambapo Mara nyingi ukiangalia blog zetu utakuta kuna msululu wa archives, msululu wa previous posts (Last posts) basi inaleta karaha kubwa (Picha Mbaya) kutokana na hiyo misululu na hii inaendana na kama mtu ukiwa una posts nyingi za zamani!

Pia tukiangalia blog zetu ktk Archives siku zote posts zile mpya zinakuwa chini na za zamani zinakuwa juu sasa baada ya kuweka code mpya za leo zitakufanya blog yako iwe na uwezo wa kuonesha ktk Archives Post mpya kwanza na kufuatia na post za zamani!!

Sasa jawabu la hilo swali au tatizo mwisho wake ni leo 25th April 2006 11:19:30am GMT+1 ambapo nakuja na code ambazo zitaondoa kabisa hiyo misululu isiyo kuwa na mwisho!

Yafuatayo ni maelekezo ya kufanya:

1: Sign In ktk Blog yako.

2: Ukifika ktk Dashboard, Click Change Settings alafu tena click Template.

3: Ukiwa ndani ya Template tafuta wapi yalipo haya maandishi,haya ni maandishi yaliyopo ktk template yangu sasa nina uhakika asilimia 99.99 ya kwamba ktk blog zenu kutakuwa na kitu kama hiko hiko. kwa kifupi, haya maandishi yapo mwisho mwisho wa code za blog zenu sasa mkifika ktk template nenda chini (mwisho wa code) na uanze kuangalia wapi hayo maandishi yalipo.

4: Baada ya kuyapata, Badilisha (Futa) maandishi yoyote yanayo endana na Archives au Previous Post (Last Posts) na nawaomba muweke hizi code.
Hizi code ni za Archives pamoja na Previous Posts (Last Posts) sasa ukiwa unafuta code kumbuka kuweka code zitakazo kwenda kuziba pengo lililowachwa wazi pia kuwa muangalifu usije kufuta code zisizo endana na Archives au Previous Post (Last Posts).

Kama kukiwa na tatizo au maswali yoyote nitafurahi kuweza kuyajibu au kutoa ushauri wowote, cha kufanya ni kuniandika hapa ktk hii blog au nitumie e-mail na nitakujibu asap.

Nashukuru.


Wednesday, April 12, 2006

Je unafahamu hii?
Je ulidhani ya kwamba mtu kutokuwa na password yako au jina unalotumia hawezi kujua code zilizo tengeneza blog au website yako? Kama ulikuwa una waza hivyo naomba usiwaze tena maana kuna njia moja wapo ambayo mimi ninafikiri njia hii ni kutokamilika kwa internet (Ubaya wa internet).

Sasa ebu tuangalie ni jinsi gani utakavyo gundua code za mtu mwingine zilizotengeneza blog yake! Kwanza kabisa naomba u-right click mouse yako alafu tafuta maandishi yaliyoandikwa View Source baada ya kuyapata jaribu ku-click (Ingia) ktk hayo maandishi basi baada ya hapo utajua code zilizotengeneza hiyo website au blog pia utajua mambo mengi zaidi ukiziona hizo code.

Sasa basi kutokana ya kwamba internet ni chombo kizuri na kibaya pia nimeweza kuwaletea dawa itakayo ondoa hilo tatizo. Dawa yenyewe itaenda kutibu pale palipo na tatizo ambapo ni kuweza kuzima uwezo wa mtu yoyote kuweza ku-right click akiwa ndani ya blog au website yako!!

Yafuatayo ni maelekezo ya kuweza kuzima right click mouse:

1: Sign In ktk Blog yako

2: Ukifika ktk Dashboard, Click "Change Settings" alafu Click sehemu ya "Template".

3: Ukishafika kwenye Template tafuta wapi yalipo haya maandishi: <body>

4: Baada ya kuyapata hayo maandishi chini yake weka haya maandishi:

Kutokana na ya kwamba blog inakataa kuonesha hizi code naomba bonyeza hapa kuweza kuzipata hizi code.

5: Baada ya kuzipata hizo code fanya kama nilivyo elekeza hapo juu (3 - 4) alafu mwisho wake naomba click save template changes alafu click republish your blog.
Kuanzia sasa utakuwa umeweza kuzuia watu wasione viungo vinavyotengeneza blog au website yako!!!

Kuanzia leo ukitaka ku-copy kitu chochote kwanza chagua cha kuweza ku-copy (select, highlight) alafu unabonyeza ctrl+c au ukitaka ku-paste kitu chochote utabonyeza ctrl+v. Ninapo andika ctrl+v au ctrl+c nina maanisha kwanza bonyeza ctrl ukifuatia na v au c kwa wakati mmoja yaaani usiachie kile ulicho bonyeza mwanzo ukiwa unabonyeza cha pili. Naomba angalia keyboard yako.

mwisho, kumbuka hii inazuia website au blog yako tu hivyo basi utakuwa na uwezo wa ku-right click ktk website nyingine au blog nyingine.

Ukitaka kuweza kuweka ulinzi mzuri ktk computer yako kumbuka kununua software zitakazo linda computer yako, unaweza ku-download vitu vifuatavyo ambavyo ni bure (Download zote mbili):

1: Malicious Software Removal Tool

2: Windows Defender (Beta 2)

3: Kwa ulinzi zaidi baada ya ku-download hivyo vitu hapo juu, wale wanaotumia window xp mnaweza kuimalisha ulinzi kwa kubonyeza Start --> Control Panel --> Security Center--> Na uweze kuona kama Firewall ipo ON, Microsoft Automatic updates ipo ON, Virus Protection ipo ON. Kama hivyo vitu vipo OFF unaweza kuviweka ON na ktk Firewall weka ON alafu chagua don't allow exceptions na mwisho click OK. Kwa ujumla ukifika ktk Security Center utapata maelezo zaidi ya kufanya. Pia kama unatumia window xp service pack1 nakushauri nenda microsoft. na uweza ku-download window xp service pack2 kwasababu sp2 ni imara zaidi kwa ulinzi wa computer yako kuliko sp1.

Software nyingine ambazo ni bure zitakazo weza kulinda computer yako ni (Chagua moja kati ya hizi):

A: Lavasoft Ad-Aware SE

B: Spybot Search & Destroy (S&D)

Kama una pesa ya kununua software mimi naunga mkono (napendekeza) hii bonyeza hapa kusoma zaidi maana hii ni imara sana.

Kumbuka ya kwamba kama ukiwa na software moja usichanganye na nyingine maana zitakuwa zinaingiliana kulinda computer yako na kuweza kufanya hackers kuiba siri zako zilizopo ktk computer yako. Pia kumbuka usi-download kitu chochote usicho kijua ata kama ni kizuri kiasi gani soma kwanza maelezo yote na ndio download au usifungue e-mail yoyote kama hamjui mtu aliye ituma.

Pia unaweza kubonyeza tools hapo juu-->Internet Options-->Security: Internet-->Medium, Local Intranet--> Medium, Trusted Sites--> Medium, Restricted Sites--> High kila unapokuwa ukibadilisha click apply.
Ukiwa hapo hapo ktk Internet Options--> Privacy: Medium High alafu chagua block popups maana popups nyingi ni mwanzo wa spyware na virus wengine. Kama ukitaka kuruhusu popups ambazo unaziamini siku zote bonyeza Ctrl na wakati huo huo click ktk sehemu husika.

Unaweza kujifunza zaidi kwa kuangalia video zifuatazo bonyeza hapa pia angalia hii video.

Kwa habari zaidi kuhusu software mbali mbali bonyeza hapa au unaweza kutembelea microsoft.

Ukiwa na maswali zaidi kuhusu hii nakala naomba niandikie na nitakujibu asap.


Nashukuru.


Wednesday, April 05, 2006

JAWABU LIMEPATIKANA:

Baada ya kukaa chini muda mrefu na kuweza kugundua code zinazo ondoa Blogger NavBar (Ile Search Box iliyopo juu ya blog yako) hii ni kutokana watu wengi hawaipendi Blogger NavBar. lakini kutokana ya kwamba hakuna njia nyingine ya mtu ku-search kwa urahisi nakala ulizo andika nyuma (zilizopita) ilibidi watu wengi waache Blogger NavBar kama ilivyo!!

Sasa nimerudi tena na kuweza kugundua code mpya zitakazo wezesha mimi na wewe kuondoa Blogger NavBar na vile vile kuendelea kuwa na uwezo wa ku-search nakala zako zilizo pita.

Yafuatayo ni maelekezo ya kufanya hivyo:

A: Fanya yale maelekezo niliyo andika mwanzo ili uweze kuondoa Blogger NavBar naomba usome kupitia hapa. , Baada ya kuweza kuondoa Blogger NavBar fuata haya maelekezo:

B: Copy code zifuatazo (Chagua moja wapo la kundi yafuatayo hapa chini kutokana na mapendekezo yako) na nenda ktk Sign in ktk Blog yako-->Dashboard-->Change Settings-->template na uweze kuchagua ni mahali gani unataka hii Search Box yako iweze kutokea. Baada ya kuchagua na kupata sehemu ya kuweka code zako (sehemu ya kutokea search box yako) Paste code ulizo zi-copy. Kama unataka kuona search box yako imekaa sehemu unayo itaka (unayo ipenda) click Preview kabla ya ku-click Save Template Changes au ku-Click Republish your Blog. Endelea kufanya hivyo mpaka utakapo pata sehemu unayo ipenda.

C: Katika hizi code utakuta neno YOUR DOMAIN NAME futa hayo maandishi na weka anuani ya website yako yaani mfano: value="YOUR DOMAIN NAME" name.. na iwe hivi: value="http://vijimamboz.blogspot.com" name hivyo ndio mfano kama ingekuwa ni mimi naweka hizo code sasa badilisha kutokana na anuani yako ya blog. Fanya hivyo popote pale utakapo ona hilo neno ktk code zifuatazo hapa chini.

D: Click Save Template Changes alafu Click Republish your Blog.

Kutokana ni vigumu kuweza kuweka hizo code hapa maana zinakataa kuji-publish na kutokea kama page, nawaomba msome kupitia hapa. (Right click na chagua open in new window) ili ifunguke ktk page nyingine.

utaitaji ms-word kufungua hili file.

Kumbuka watu wengi hawaipedi Navbar kutokana inazuia kuweza kuweka vitu vingi ktk site yako mfano: calendar, saa na vitu vingi ambavyo vinaitaji viwepo juu ya site yako, Vile vile inaleta picha mbaya.

Kama una maswali au Tatizo zaidi kuhusu hili swala naomba niandikie na nitakujibu asap.

Nashukuru.

Monday, April 03, 2006

Baada ya uchunguzi wa siku nyingi na wa hali ya juu nimegundua jawabu la kuondoa Blogger NavBar (Sehemu ya juu kabisa ya Blog yako inayo onesha search this blog). Hii kutokana na ya kwamba watu wengi uwa wanachukizwa na jinsi hiyo NavBar ilipo.

Jawabu la hili swali ni:

1: Sign in ktk Blog yako.

2: Ukifika ktk Dashboard, Click "Change Settings" alafu Click sehemu ya "Template".

3: Ukishafika kwenye Template tafuta wapi yalipo haya maandishi:
link rel="stylesheet" type="text/css" href="style.css"/>
/*

au blog zingine kuna maandishi haya:
style type="text/css"
/*

Hapa kwenye template ni sehemu inayo ifadhi code ambazo zinazotengeneza blog yako. Sasa basi mara nyingi hayo maandishi yapo mwanzo mwanzo wa code zinapoanzwa kuandikwa. Sasa usiangaike kwenda chini zaidi au katikati, Wewe Unapofika kwenye template tu angalia mwanzoni na utaona hayo maandishi.

4: Baada ya kupata hayo maandishi naomba chini yake weka haya maneno: #b-navbar{ margin-top: -500px;}

Kumbuka haya maneno ndio dawa ya kuondoa NavBar. Narudia tena dawa ni #b-navbar{ margin-top: -500px;}

Baada ya kumaliza ni lazima maandishi yaonekane kama hivi:
link rel="stylesheet" type="text/css" href="style.css"/>
#b-navbar{ margin-top: -500px;}
/*

Wenye blog zingine zionekane kama hivi:
style type="text/css"
#b-navbar{ margin-top: -500px;}
/*

5: Mwisho: Click Save Template Changes alafu Click Republish your Blog.

Kama una maswali au Tatizo zaidi niandikie.

Nashukuru.

Sunday, February 12, 2006

Je walipenda somo la Biology? Kama jibu ni ndio, Ninawaletea hii link ambayo inafundisha somo la Anatomy.

Click ktk haya makundi yafuatayo (popote ktk makundi 4 ya hapa chini) na utapelekwa kwenye site nyingine ambayo inafanana kama yalivyo haya makundi:
Autopsy Programme 1 - Circulation
Part 1
Part 2
Part 3
Part 4

Autopsy Programme 2 - Cancer
Part 1
Part 2
Part 3
Part 4

Autopsy Programme 3 - Poisoning
Part 1
Part 2
Part 3
Part 4

Autopsy Programme 4 - Ageing
Part 1
Part 2
Part 3
Part 4

Baada ya ku-click na kupelekwa ktk hiyo site nyingine basi uta-click ktk kila sehemu (Part 1 - 4 ktk kila kundi) ambapo utapata hayo mafundisho kwa video, Unabidi uwe na Windo Media Player kucheza hizo video.

Nataka kuwaonya wale "Wenye roho ndogo" wasiweze kuangalia hizi video maana kuna miili tofauti tofauti ya binadamu walio kufa inayotumika kufundishia.

Miili yote hii imetolewa na marehemu husika kwenda kwa the Institute for Plastination, Germany na hao marehemu kabla ya kifo chao walikubali kwa miili yao kutumika kwa sababu ya masomo tu.

Kumbuka kuweza kuangalia hizi video sio lazima uwe doctor au mwanafunzi anae taka kuwa doctor bali waweza kuangalia kama unataka kujifunza zaidi kuhusu mwili wako na wa binadamu kwa ujumla!

Natumai utaweza kujifunza mengi.