Thursday, May 18, 2006


HISTORIA YA AIRBUS A380 NDANI YA UK
Ndege ya abiria aina ya Airbus A380 yenye viti vya abiria 555 ambayo ni kubwa kuliko zote ulimwenguni imeweza kuingia ktk historia ya kuwa ni ndege ya kwanza ya aina hiyo kutua ktk ardhi ya Uingereza ktk uwanja wa ndege wa Heathrow hii leo 18/05/2006 saa 13:20 mida ya Uingereza ikitokea Berlin, Germany.

Maandalizi ya kuwezesha ndege hiyo kutua ktk uwanja wa Heathrow imewagarimu waingereza ( British Airports Authority) jumla ya 450 Million pounds na pia imetua ktk sehemu impya ( Inayo julikana kama pier 6 ktkTerminal 3) iliyo jengwa na kugarimu jumla ya 105 Million pounds.

Airbus A380 itakuwa ni mshindani mkubwa wa ndege za Boeing, na kuonesha Boeing wapo ktk ushindani nao wametengeneza ndege aina ya 787 Dreamliner kuweza kushindana ambayo inategemewa kuingia ktk soko ifikapo mwaka 2008 na kuweza kubeba abiria kati ya 200 mpaka 350.

Jumla ya gharama zilizo wezesha kutengeneza ndege ya Airbus A380 ni 6 Billion pounds ambapo mpaka sasa kampuni ya Airbus S.A.S imepokea order karibia 159 kutoka kwa mashirika 16 ya ndege zinazotaka kununua aina hii ya ndege.

Bonyeza hapa kusoma orodha ya makampuni na idadi ya ndege walizo order.

Bonyeza hapa kuona video mbali mbali za Airbus A380 pia kama ukitaka kuangalia video nyinginezo zinapatikana kwa kubonyeza hapa.

Mwisho, ingawa hii ni kama historia lakini imeleta mitazamo tofauti ambapo kuna makundi mawili, yanayo kubaliana na technology hii na wanao ipinga kutokana na sababu za mazingira.

5 comments:

Mija Shija Sayi said...

Mk,
Hivi kwa Afrika unadhani ni wapi angalau ndege kama hii inaweza kujaribu kutua? ninamaanisha uwezo wa uwanja.

Lingine, mbona somo la baiolojia haliendelei tena, lirudishe tuwe tunakuuliza-uliza maswali.

zemarcopolo said...

kwa sababu fulanifulani mimi najiunga na upande wa wale wanaopinga kuwepo kwa midege kama hii....joto duniani linaongozeka na ni wakati kwa viumbe vyote vinavyoishi duniani vikiongozwa na sisi binaadamu kushirikiana kutafuta mbinu za kukabiliana na hali hii.kiasi cha uharibifu kinachosababishwa na ndege hii ni zaidi ya ndege tano zinazoweza kubaba abiri 150!!!mimi nahofia.

MK said...

Damija, Kuhusu uwezo wa uwanja naona labda kwanza tuweze kufanya marekebisho ktk viwanja vyetu na ni mataifa machache ndio wakuwa na uwezo huo kutokana na sababu za kifedha na kiuchumi.

Kuhusu ombi lako kuhusu somo la biology nitalifanyia kazi.

Hii ndege naipenda sana ingawa nipo 49 - 51 na nipo 51 ktk maswala ya mazingira sababu tukizidi kutengeneza vitu vitakavyo haribu mazingira yetu ni wapi tutaenda kuishi? maana wote tunajua hakuna sehemu nyingine ya kuishi binadamu zaidi ya hii dunia (planet earth) na safari bado ni ndefu kuweza kugundua planets nyingine zitakazo wezesha binadamu kuishi hivyo naungana na zemarcopolo pamoja na wana mazingira.

Nashukuru kwa kutembelea Vijimamboz.

Copyright 2006 MK

zemarcopolo said...

vijimamboz lazima tuvitembelee kwa sababu kwenye blog zote tunasoma kuwa mzee wa vijimamboz ndio pele wa blogas.....
kazi njema!

msangimdogo said...

Sina hakika kama kutakuwa na walau asilimia 75 ya watu kutoka Afrika ambao watakuwa tayari kuunga mkono maendeleo kama haya sababu hayawezi kuwasaidia. Sana sana nadhani jamaa wanazidi kuongeza uwezo wa zana zao za kuingizia silaha huku barani kwetu, mtu akija mkupuo mmoja anakuwa keshagawa za kutosha anaondoka na kusingizia ruti hiyo hailipi kumbe alishafanya vitu vyake.

Lakini pia nina wasiwasi huenda wakaona kuna vitu vingi vya kuchukua huku wakayatuma hayo madege na kwakuwa hakutakuwa na sehemu za kujenga, basi watazinunua serikali zetu ziwabomolee wananchi wake vibanda vyao ili kupisha ujenzi wa uwanja mpya, kama sio kutoa kibali cha kipande cha bahari kukaushwa kwa ajili ya kukaribisha mwekezaji anayekuja kutujengea uwanja wa kimataifa wa ndege.

Ni mtizamo tu lakini