Tuesday, May 16, 2006

Kama ukitaka blog yako ipendeze zaidi, basi unaweza kuweka hizi code ili kuweza kufanya scrollbar yako kubadilika rangi au iwe na rangi tofauti tofauti. Unaweza kuangalia scrollbar ktk blog yangu na kuona ninacho sema.

Unaweza kubadili rangi tofauti tofauti kutokana na mapendekezo yako, na utaweza kufanya hivyo ktk sehemu zenye maandishi kama #FFFFFF; #6DA4FF; #ACA899; black; #FFFFFF; na kufuta #FFFFFF, #6DA4FF, #ACA899, black au #FFFFFF na kuandika rangi unayotaka eidha kwa kutumia code kama nilivyo andika mwanzo au kwa maandishi mfano pink, green, red, n.k.

Kumbuka ukiandika kwa code au kwa maandishi andika kwa usahii na kwa kiingereza tu na msifute alama hii ; yaani ukiandika red iwe red; au #ff0000; hivyo ndivyo ingekuwa kwa kutumia code nikiwa nina maanisha rangi nyekundu.

Yafuatayo ndio maelekezo ya kufanya:

1: Sign In ktk Blog yako

2: Ukifika ktk Dashboard,Click->Change Settings->Template

3: Ukifika ktk template, tafuta wapi yalipo haya maandishi head yakianza na tag < na kuishia na tag > na baada ya kuyapata hayo maandishi chini yake weka code zifuatazo.

4: Mwisho, click save template changes alafu click republish your blog.

Na hapo utakuwa umemamaliza kila kitu.

2 comments:

Reginald S. Miruko said...

ndugu yangu naona mambo yako n mazito. Mkono wako unaonekana katika blogu nyingi sasa keep it up

MK said...

Nashukuru ndugu Miruko kwa maneno yako na nashukuru kuona umetembelea vijimamboz.

Nakutakia kazi njema.

Nashukuru,
Copyright 2006 MK