Saturday, May 06, 2006


NI NANI WA KUOKOA DARFUR NA AFRIKA?

Hapa uliwenguni ni mahali pazuri na pabaya kuishi, Ni pazuri kama tukiwa na Amani na Upendo na Vile vile kunakuwa ni pa chungu kama Amani na Upendo ukitoweka.

Dhumuni la nakala hii ni kuonesha au kuuliza ni nani atakae okoa Wananchi Darfur na Afrika kwa ujumla hasa hasa watoto na akina Mama? Kwa Mfano hapo Darfur ni tatizo la siku nyingi likiwa linaendelea kila siku na Viongozi wetu wa hii dunia wakibaki kuliangalia tu kama vile hawalioni!! Wanabaki wakiliangalia na kuacha ma-million ya wananchi wakiteseka na kufa kwa njaa au kuuana wenyewe kwa wenyewe.

Vile vile hata Serikali yenyewe ya Sudan inabaki midomo imefunga na kuliangalia hilo swala ata pia wakiweza kudhamini ata wale magaidi (The Janjaweed) wanao ua kila siku watoto, wanawake, na wanaume!!

Nchi nyingi za Afrika wanajifanya kama hawalioni hili swala na kuna wakati walijifanya wanaona na kupeleka majeshi ya AU (Askari 7,000 tu) lakini cha kushangaza hayo majeshi hayafanyi chochote kuzuia Vifo vya watoto, wanawake, na wanaume.

Dunia inajifanya inaona na kutaka kusaidia lakini inapofika kusema kuiwekea Serikali ya Sudan Vikwazo na kupeleka majeshi ya UNO kulinda Amani, Utaona baadhi ya nchi zinazopata maslahi toka Sudan zikizua hilo pendekezo hii ikijumuisha nchi ya China ambayo imewekeza zaidi ya 3 Billion US Dollars ktk Mafuta ya Sudan na hizo hizo pesa ndizo zinazo dhamini Silaha zinazo leta hivi Vifo.

China imekuwa nchi ambayo haifuati haki za binadamu na Sheria ambapo kutokana siku hizi imekuwa Super Power ktk hii dunia basi matumizi yake pia yanakua ambayo yanafanya kutafuta soko la mahitaji yake bila hata ya kufuata sheria (Kufumba Macho mabaya yafanywayo na Serikali zinazo mpatia hayo mahitaji) hii ikijumuisha Kenya- Haikemei Rushwa inayo endelea, n.k, Zimbabwe- Haikemei uvunjwaji wa haki za binadamu, n.k, Sudan- Haikemei Uvunjwaji wa haki za binadamu, na pia ndio inazuia muswada usipitishwe ktk Umoja wa mataifa kwakuwa ina kura ya Veto, Chad- Haikemei uvunjwaji wa haki za binadamu na watu wanakufa na njaa huku kiongozi wa nchi hii akiishi maisha ya kifalme na kununua magari ya kifahari!! Hii mifano sio kwa nchi za Afrika tu bali ktk nchi nyingi hapa duniani, Yaani nina mifano mingi tu hii ikijumuisha mataifa mengi hacha China tu.

Mpaka nina andika hii nakala baadhi ya vikundi ndani ya Sudan havikuweza kuweka sahii ktk makubaliano ya Amani!!

Kwa Ufupi tu hapa nina uliza ni nani atakae kuja kutukomboa ktk haya matatizo tuliyo nayo Afrika?

Ni nani atakae kuja kuokoa watoto, Wakina Mama, Wakina Baba wa Darfur?

Kwanini wanaendelea kuuza Silaha kwa nchi za Afrika zenye machafuko zinazo fanya kuuana wenyewe kwa wenyewe?

Wako wapi Viongozi wa Afrika na hii dunia?

Mungu Ibariki Tanzania, Mungu Ibarika Afrika.

Nashukuru.

1 comment:

mzee wa mshitu said...

Bwana MK,
Nashukuru kwa kufahamu huu upande wa pili wa makomredi wetu wa China, nilikuwa silifahamu hili nimekuwa nikiwaangalia kama watu ambao ni wellwishers ni wajamaa ni wapenda watu kumbe nao wako kama Wamarekani tu sasa haya mambo ya kuisaidia Sudan si balaa, anyway bado najikunja kujua zaidi mambo ya China kwa upande huo.