Tuesday, May 09, 2006

NA NYINGINE HIYO!!
Leo nawaletea code nyingine kwa wale wenye blog ndefu au blog za picha ambazo ni ndefu.

Code hizi ni kuwawezesha wasomaji wenu kuweza kupelekwa juu (Mwanzo) pale wafikapo mwisho bila ya kuangaika kwenda juu. Mfano wake upo ukiangalia chini ya hii blog (Vijimamboz) utaona kuna kijisehemu kina kwambia rudi juu na uki-click hapo unakwenda juu.

Maelekezo ni kama kawaida, Ambayo ni:
1(a): Sign In ktk Blog yako

1(b): Ktk Dashboard,Click->Change Settings->Template

1(c): Ukifika ktk template, Chagua ni wapi unataka hiyo button iweze kukaa (Ni vizuri ukiweka chini kabisa maana wasomaji wenu wakishafika mwisho wa blog tu waweze kukibonyeza na kupelekwa juu) na alafu muweke hizi code.

1 (d): Mwisho, click save template changes alafu click republish your blog.

Na hapo utakuwa umemamaliza kila kitu.

6 comments:

Martha Mtangoo said...

MK naomba unibadilishie blog yangu nayo minonekane ya kisasa, nahitaji kuwa nan kijiwe cha ambacho nitakiita CHINI ya Mti, user name marthadm, password majira. ukisooma ifute hiyo.

MK said...

Habari zako dada yangu,

Usiwe na shaka nitalifanyia kazi hili swala.

Alafu nimebadilisha password yako na nimekutumia password mpya ya blog yako ktk e-mail yako naomba iangalie.

Nimefanya hivyo kwasababu umeweka wazi password yako muhimu (Siku nyingine naomba usifanye hivyo) sababu watu wanaweza kuingia na kubadilisha password na ukashindwa kutumia blog yako tena na wao wakatumia jina lako kufanya mabaya.

Nashukuru,
Copyright 2006 MK. All rights reserved.

Sultan Tamba said...

Salama? Nimetembelea blogu yako na nimeipenda,pia nimependezewa sana na moyo wako wa kusaidia wengine na nakiri kwamba kuna ujuzi kidogo niliipa kwenye mafundisho yako nikautumia. Ukitembelea yangu utaona nilipofikia. Ninayo maswali ya kunijibu ili unisaidie zaidi. Nayo ni haya hapa.
Ukiangalia blogu yangu, ile picha ya kwenye profile niliiweka mwanzoni wakati naanza kutengeneza, leo nimejaribu kuibadilisha nimesahau njia. Naomba nisaidie nitaibadilisha kwa kupita wapi na wapi.
2. Nawezaje kuweka rangi kwenye Headline zangu?
3. Nataka kufuata maelekezo yako kuhusu kuondoa ile bar ya juu, lakini nitawezaje kuweka muda huko juu baada ya bar kuondoka?
Nashukuru, hayo ni machache, lakini unaweza kunisaidia na mengine kadiri unavyoona blogu yangu ilivyo.

Sultan Tamba said...

Nilipotaja Muda kuweka juu ya hiyo Bar nitayoondoa, nimemaanisha kuweka saa au nawezaje kuweka vitu vingine vizuri zaidi?

MICHUZI BLOG said...

mk, najua sijawahi kutia neno humu. lakini elewa nafuatilia sana blogu yako (na wote wanaontembelea) kila siku. ahsante kwa darasa unalolitoa kila wakati. pia sikujua kwamba blogu yangu ni ndefu. hivi kipimo ni nini hasa? na je inaboa amaniendelee na staili hiyo. naomba ushauri wa kitaalamu

MK said...

Blog yako ni nzuri sana tena sana na ni moja ambazo zinaitaji heshima kubwa sana.

Endelea na style hiyo hiyo kwa kutupa burudani sisi wasomaji wako wa ndani na nje ya Tanzania. Lakini labda ungeweka hicho ki-button ili kiweze kumpeleka msomaji juu akiwa amemaliza kusoma afikapo mwisho.

Blog yako ni kama Ubalozi wa Tanzania ambao watanzania wote tunakutana.

Yaani ile blog ni nzuri sana na nina uhakika baada ya miaka kazaa ijayo inaweza kupata mafanikio kama ya akina google, n.k kwa kupanuka kwa zaidi na kuwa na wasomaji wengi au ata kuweka matangazo ya ndani na nje ya nchi na ukawa unawalipiza pesa.

Mwisho, Endelea kuweza kuweka burudani hii sababu jamii inakutegemea ktk mchango wako.

IssaMichuzi.blogspot.com Idumu daima.

Nashukuru,
Copyright 2006 MK

Nota Bene: Ndugu yangu Sultan Tamba tunaweza kuwasiliana zaidi kesho au siku yoyote ukipata muda kupitia yahoo messenger na address yangu ni akathepretender@yahoo.co.uk na hapo tutafanya hayo marekebisho. Nashukuru.